7.1 C
New York

Chart: Imani potofu kuhusu TB Tanzania

Published:

Na Faraja Masinde, Gazetini

Machi 24, ya kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine duniani kiadhimisha siku ya Kifua Kikuu(TB).

Kwa hapa nchini Takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa kumekuwapo na ongezeko la watu wanaogundulika kuwa na TB kila mwaka.

Takwimu za miaka minne mfululizo kuanzia 2018 hadi 2022 zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la watu 25,373 waliogundulika kuwa na TB.

Hii ni sawa na kusema kwamba kila mwaka wagonjwa wamekuwa wakiongezeka.

Wakati hali ikiwa hivyo wataalamu wa afya wanadokeza kuwa changamoto kubwa imekuwa katika maeneo ya mijini.

Dk. Mbarouk Seif ni Mratibu wa Kifua Kikuu(TB) na Ukoma Jiji la Dar es Salaam ambapo anataja baadhi ya changamoto pamoja na mikakati ya baadae katika kudhibiti ugonjwa huo.

“Moja ya sababu kubwa inayochochea TB kwa maeneo ya mijini ni misongamano, ukosefu wa hewa safi, watu kutokuchukua tahadhari wakati wa kukooa na sababu nyingine.

“Ikumbukwe kwamba malengo ya Mpango Mkakati ya Tanzania ni kupunguza maambukizi mapya ya TB kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2025 ikilinganishwa na hali ya mwaka 2015.

“Pia vipaumbele vingine vya nchi ni kuwafikia watu wote ambao hawajagundulika kiwa na TB na kuwawek kwenye matibabu. Hii inaenda sambamba na kuboresha teknolojia za upimaji, kuhusisha watoa huduma katika vituo binafsi yakowemo maduka ya dawa na kushirikisha jamii na watoa huduma katika ngazi ya jamii,” anasema Dk. Seif.

Hata hivyo, imani potofu nayo ni sababu nyingine ambayo inachelewesha udhibiti wa TB nchini.

Dk. Linda Mutasa ni Mratibu wa Kifua kikuu Wilaya ya kihuduma ya Mnazi Mmoja ambapo anasema kiwa: “Hakuna Uhusiano wowote wa kifua kikuu na kurogwa hivyo watu wanatakiwa kuacha dhana potofu pindi wanapopata Dalili za Kifua kikuu hivyo mtu anavyopata dalili ni Vyema akafika katika vituo vya kutolea huduma.

“Moja ya dhana potofu ni kuwa kila mwenye ugonjwa wa TB ana UKIMWI na ikumbukwe kuwa TB siyo ugonjwa wa kurithi, hivyo watu wanatakiwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya,” anasema Dk. Linda.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img