7.1 C
New York

Infographic| Ilani ya CCM ilieleza nini kuhusu watu wenye ulemavu?

Published:

Na Jackline Jerome,Gazetini

Watu wenye ulemavu ni moja kati ya makundi muhimu na maalumu katika jamii, hata hivyo, wakati mwingine limekuwa likikosa nafasi katika nyanja mbalimbali.

Hii huelezwa wakati mwingine kukosekana kwa watu wa kulisemea kundi hili muhimu.

Takwimu za Benki ya Dunia (WB) za mwaka 2020 zinaonyesha kuwa asilimia 15 ya watu duniani wana ulemavu nakwamba wengi wao wako katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.

Kiwango hicho kinakadiriwa kuwa ni karibu watu 200 wana aina ya ulemavu.

Hii ni sawa na kusema kwamba katika kila watu watano wenye ulemavu basi mmoja wao ana ulemavu makubwa.

Upande wa Tanzania, kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) zinaonyesha kwamba katika sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 kiwango cha watu wenye ulemavu ni asilimia 5.8 ya watu wote. Kiwango hicho ni zaidi ya watu 2,000,000 kati ya 44,929,002.

Ikumbukwe kuwa takwimu hizo ni kabla ya sense ya mwaka 2022, ambayo bado haijaweka bayana kuhusu idadi ya watu wenye ulemavu nchini.

Ni bayana kwamba kote duniani walemavu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ile ya elimu duni, kukosa huduma za afya, ujira mdogo na umaskini uliokithiri.

Hayo yanashuhudiwa wakati ambao ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UN-SDGs) imekuwa bayana kuwa kufikia 2030 ulemavu hautakuwa kigezo au sababu itakayomzuia mtu kushiriki katika mipango mbalimbali ya maendeleo ili kufurahia haki zake kama binadamu.

Pia, mkataba wa UN kuhusu watu wenye ulemavu (CRPD) unasisitiza juu ya ujumhishwaji wa watu wenye ulemavu katika jamii.

Ilani ya CCM inaeleza nini

Katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2020 hadi 2025 ukurasa wa 146 inabainisha juu ya mambo kadhaa yatayo tekelezwa na chama hicho kwa kipindi hiki cha miaka mitano kwa watu wenye ulemavu.

Chama hicho kinaeleza kuwa ustawi wa watu wenye ulemavu ni muhimu katika kuleta maendeleo yenye uwiano katika jamii. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasisitiza usawa na haki.

Aidha, kinaongeza kuwa, kimeendelea kuwatambua watu wenye ulemavu na kuwapatia kipaumbele katika masuala mbalimbali ikiwemo ajira na uteuzi, ujenzi wa miundombinu rafiki, huduma bora za afya, uzazi salama.

Eneo jingine ni katika marekebisho na utengamao pamoja na kukomesha vitendo vya ukatili na unyanyasaji vinavyoshusha utu wao vikiwemo ubaguzi, uonevu pamoja na mila potofu.

Je ipi ilikuwa ahadi?

“Kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Na. 9 ya Mwaka 2010 ili kuendana na mabadiliko ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiteknolojia.

“Kuvifufua vyuo vya ufundi maalum ili viweze kuwapatia mafunzo maalum ya stadi za kazi na utengamano (rehabilitation) watu wenye ulemavu ili waweze kuajiriwa au kujiajiri.

“Kuboresha rejista ya watu wenye ulemavu itakayotoa taarifa sahihi za watu wenye ulemavu ili kuimarisha utoaji wa huduma na misaada. Kubuni na kutekeleza mikakati ya kuwawezesha kiuchumi watu wenye ulemavu ili waweze kutoa mchango wao katika maendeleo ya Taifa,” inaeleza ilani hiyo.

Inaongeza kuwa jambo jingine ambalo litatekelezwa na chama hicho kwa watu wenye ulemavu katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 ni kujenga, kusimamia na kuhimiza uwepo wa miundombinu rafiki ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanafikia huduma mbalimbali kwa urahisi.

“Kubuni na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuwezesha watu wenye ulemavu kujiajiri na kuajiriwa, kuimarisha udhibiti wa vitendo vya kikatili na unyanyasaji vinavyoshusha utu na hadhi ya watu wenye ulemavu vikiwemo ubaguzi, uonevu na mila potofu; kuboresha na kusimamia utoaji wa msaada wa kisaikolojia kwa watu wenye ulemavu,” inabainisha ilani hiyo ya CCM.

Je utekelezwaji wa ahadi hizi unafanyika?

Zaidi soma usanifu wetu hapo juu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img