Na Anoth Paul, Gazetini
Ajali zitokanazo na pikipiki zimesababisha idadi kubwa ya wagonjwa katika Taasisi ya Mifupa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Asilimia 70 ya wagonjwa wanaofikishwa katika Hospitali hiyo ni wale watokanao na ajali hizo.
Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) inalojukumu la kuhudumia wagonjwa wenye shida zinazohusiana na matatizo ya mifupa kwa pande mbili tofauti kuna yale matatizo ya mifupa yatokanayo na magojwa au watu kuzaliwa nayo na upande wa pili ni matatizo ya mifupa kutokana na ajali mbalimbali tunazokumbana nazo.
Katika hali sio kawaida, kwenye taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Dk. Respicius Boniface zinaeleza kuwa katika taasisi hiyo idadi ya wagonjwa wenye matatizo ya mifupa imeegemea zaidi katika upande wa ajali zitokanazo na pikipiki maarufu kwa jina la (Bodaboda), Dk. Boniface anasema ukiacha wagonjwa wenye matatizo ya mifupa bila kuhusisha ajali za pikipiki, Hospitali hiyo inapokea zaidi ya asilimia 70 ya wagonjwa watokanao na ajali za pikipiki pekee kama anavyoeleza Dkt. Boniface
Kwa siku Taasisi ya MOI hupokea majeruhi kuanzia 10 hadi 15 wanaotokana na ajali za pikipiki ikiwa sawa na aslimia 70 ya wagonjwa wote hospitalini hapo na kwa mantiki hiyo wagonjwa zaidi ya 300 kwa mwezi ambayo ni sawa na wagonjwa 3,600 kwa mwaka hupelekwa hospitalini hapo na hii ni kutokana na takwimu alizozitoa Mkurugenzi huyo tarehe 6, Juni 2022 wakati akizungumza na vyombo vya habari kwenye ukumbi wa mafunzo yaliyokuwa yakiendeshwa kwa Madaktari mbalimbali nchini ili kuendelea kuboresha huduma za kuwatibu wagonjwa wa aina hiyo katika hopitali zingine za mikoani mbali na MOI pekee.
Katika mahojiano mengine aliyowahi kuyafanya Dk. Bryson Mcharo ambaye ni daktari bingwa wa mifupa na viungo kutoka MOI mwaka 2021 na chombo cha habari cha “The Chanzo” anasema“Kuna siku unapata wagonjwa watano kuna siku kumi, kwa hiyo wastani wa wagonjwa ni watano mpaka sita kwa siku wa bodaboda,” Dk. Mcharo alieleza kwenye mahojiano hayo yaliyofanyika ofisini kwake.
“Tukilinganisha majeruhi tunaowapata wa bodaboda na majeruhi tunaowapata wa ajali zingine, inaonekana bado wa pikipiki ni wengi kuliko wale wa magari na vitu kama hivyo” anaongeza kuwa: “Pia katika ripoti ya uhalifu ya mwaka 2019/2020 iliyotolewa na Jeshi la polisi katika ukurasa wa 54 inaonyesha ni wanaume ndio wahanga zaidi wa ajali hizi kuliko wanawake, huku mikoa ya kipolisi ifuatayo ikiwa na kiwango kikubwa cha ajali hizo kwa muujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi.
Kwa muujibu wa ripoti ya uhalifu ya mwaka 2020 inaonyesha ajali za piki zilizotokea mwaka 2019 zilikuwa 628 na watu waliokufa walikuwa 355 sawa na asilimia 56.5 wakati walijeruhiwa ni 526 sawa na 83.7 na kwa mwaka 2020 ajali zilikuwa 505 na waliopoteza maisha walikuwa 319 sawa na asilimia 63.1 wakati watu 422 walijeruhiwa sawa na asilimia 83.