22.9 C
New York

Visual| Mitandao ya simu ilivyopoteza wateja

Published:

Ripoti mpya ya Robo ya tatu ya Mwaka 2021 iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonyasha kuwa kumekuwa na panda shuka ya wateja wanaofanya miamala kwa njia ya simu za mkononi.

Aidha, ripoti hiyo ya miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba 2021 inaonysha kuwa wateja wa M-Pesa ndio wameonekana kupungua zaidi.

Airtel Money

Kwa mujibu wa ripoti hiyo upande wa mtandao wa Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money hadi Julai mwaka jana ulikuwa na wateja 7,037,775 idadi ambayo ilipanda kufikia 7,128,355 mwezi Agosti hii ni sawa na kusema kwamba mtandao huo ulikuwa umekusanya wateja wapya 90,580, hata hivyo hadi kufikia Septemba mwaka jana wateja hao walipungua na kubaki 7,127,854 ikiwa ni pungufu ya wateja 501.

Halopesa

Upande wa mtandao wa Halopesa nako licha yakuongeza watumiaji wake lakini hali haikuwa shwari mwezi Septemba.

Mtandao huo hadi Julai mwaka jana ulikuwa na wateja 3,488,763 idadi ambayo iliongezeka kufikia 3,571,094 mwezi Agosti hii ni sawa na kusema mtandao huo ulijizolea wateja wapya 82,331, hata hivyo hadi kufikia Septemba mwaka jana wateja hao walipungua na kubaki 3,562,883 ikiwa ni pungufu ya wateja 8,211.

Tigo Pesa

Hali ilikuwa nzuri upande wa Tigo Pesa kwani iliendelea kuvuna wateja mwezi hadi mwezi kwani hadi kufikia Julai 2021 ulikuwa na wateja 8,099,969 idadi ambayo ilishuka kidogo mwezi Agosti baada ya wateja 11,737 kupungua. Hata hivyo, idadi hiyo iliongezeka kufikia 8,150,496 mwezi Septemba, mwaka 2021.

TTCL (T-Pesa)

Katika upande mwingine ripoti hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL) ambayo imeonekana kuvuna wateja mwezi hadi mwezi.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Julai 2021 TTCL ilikuwa na watumiaji wa huduma ya T-Pesa wapatao 977,687 idadi ambayo iliongezeka mwezi Agosti na kufikia 989,580. Mafanikio makubwa yalionekana mwezi Septemba 2021 baada ya shirika hilo kufikisha wateja 1,073,023.

M-Pesa

Hali imekuwa mbaya zaidi kwa upande wa Vodacom(M-Pesa) kutokana na kupoteza wateja wengi ndani ya miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba 2021.

Takwimu za mwezi Julai 2021 zinaonyesha kuwa M-Pesa ilikuwa na wateja 13,389,162 idadi ambayo ilishuka mwezi Agosti hadi 13,151,832 sawa na upungufu wa wateja 237,330. Hali hiyo ilizidi kuwa mbaya zaidi kwa M-Pesa Septemba mwaka huu ambapo idadi ya watumiaji wake ilishuka hadi 12,660,205 ikiwa ni upungufu wa wateja 728,957 ikilinganishwa na mwezi Julai 2021.

Ezy Pesa

Mtandao uliokamilisha orodha hiyo ni ule wa Zantel kupitia Ezy Pesa ambao hadi kufikia Julai 2021 ulikuwa na wateja 590,164 idadi ambayo ilishuka hadi 587,505 sawa na upungufu wa wateja 2,659. Wateja wengi walipungua mwezi Septemba hadi kufikia 580,300 ikiwa ni upungufu wa wateja 9,864 ikilinganishwa na mwezi Julai 2021.

Mwenendo wa wateja wanaofanya miamala kwa njia ya simu Julai hadi Septemba 2021.

KampuniJulaiAgostiSeptemba
Airtel Money7,037,7757,128,3557,127,854
Halopesa3,488,7633,571,0943,562,883
Smile000
Tigo Pesa8,099,9698,088,2328,150,496
TTCL977,687989,5801,073,023
M-Pesa13,389,16213,151,83212,660,205
Ezy Pesa590,164587,505580,300
JUMLA33,583,52033,516,59833,154,761

M-Pesa kinara

Aidha, licha ya anguko hilo, takwimu zinaonyesha kuwa kampuni ya Vodacom kupitia M-Pesa bado imeendelea kuwa kinara kwa kumiliki asilimia 38.19 ikifuatiwa na Tigo Pesa yenye asilimia 24.58.

Airtel Money nayo haiko nyuma kwani ina asilimia 21.50 ikifuatiwa na Halopesa yenye asilimia 10.75, TTCL asilimia 3.24, Ezy Pesa asilimia 1.75 na Smile asilimia 0.00.

Wataalam

Hata hivyo, bado kuna maoni mchanganyiko juu ya kupungua kwa wateja hao kwani wapo wanaosema kwamba hiyo inachangiwa na kuwapo kwa tozo za miamala iliyoanzishwa na Serikali kwa ajili ya kuzaidi kusukuma maendeleo hasa elimu na afya.

Nassib Mramba ni Mtaalamu wa masuala ya Uchumia ambaye anasema kuwa sababu kubwa ni baadhi ya watu kuacha kutumia mimala hiyo ya simu kutokana na tozo na hivyo kuamua kugeukia njia mbadala zikiwamo zile za asili.

“Njia mbadala ni pamoja na kutuma fedha kwa njia ya basi au mtu kwendamoja kwa moja hatua ambayo baadhi wanaona kama inapunguza gharama licha ya ukweli kuwa siyo njia salama na inapunguza mapato kwa Serikali na ajira kwa Watanzania waliajiriwa kama mawakala,” anasema Mramba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img