LOS ANGELES, Marekani
MMOJA ya washitakiwa wanne wa mauaji ya Pop Smoke amemuomba radhi mama mzazi wa staa huyo wa muziki wa Hip hop nchini Marekani.
Blockstar aliyetajwa kuhusika katika tukio la kumpiga risasi Pop Smoke mwaka 2020, amesema hakuwa na ugomvi binafsi na msanii huyo.
Mshikaji huyo alikuwa na umri wa miaka 17 wakati anahusika katika tukio hilo. “Naweza kusema namuomba radhi mama yake Pop Smoke,” amesema.
Sambamba na msamaha huo, pia Blockstar amesema hakuwa na ugomvi wowote na Pop Smoke bali alishiriki kumuua kama sehemu ya kupata fedha.
“… mambo hutokea, na wakati mwingine huwa ni mabaya. Siyo kisingizio lakini mambo yanapokuwa mabaya ni vizuri kuyaweka wazi,” amesema Blockstar.
Kati ya washitakiwa wanne, ni wawili tu waliokuwa na umri wa zaidi ya miaka 18. Miongoni mwao ni Corey Walker aliyekuwa na miaka 19 wakati huo na alihukumiwa miaka 25 gerezani.
Keandre Rodgers aliyekuwa na miaka 18, aliachiwa huru lakini hivi karibuni mashitaka dhidi yake yalifufuliwa na kuanza kusikilizwa upya.


