23.1 C
New York

PSG yakubali dau la Garcia

Published:

BASEL, Uswis

KLABU ya PSG ya jijini Paris, Ufaransa, imekubali kuweka mezani ofa ya euro milioni 70 ili kukamilisha usajili wa beki wa Barcelona, Eric Garcia.

Ripoti zinaeleza kuwa Garcia yuko kwenye mipango ya PSG na wanajipanga kumsajili majira ya kiangazi, 2027.

Taarifa zinaeleza pia, kocha wa PSG, Luis Enrique, ambaye aliwahi kuinoa Barcelona ndiye anayeshinikiza mabosi wa PSG kumsajili nyota huyo.

Garcia ni mchezaji muhimu kwa Barcelona na mkataba wake na Wacatalunya hao utafikia ukomo mwaka 2031.

Msimu uliopita, Mhispania huyo alicheza mechi 51 za mashindano mbalimbali, akiingia kikosi cha kwanza mara 47.

Nyota huyo aliibuliwa na ‘academy’ ya Barcelona lakini aliondoka klabuni hapo mwaka 2017 na kujiunga na Manchester City. Alirejea Camp Nou mwaka 2021.

Related articles

Recent articles