23.1 C
New York

Arsenal nguvu zote kwa Kim Min-jae

Published:

MUNICH, Ujerumani

NI taarifa kutoka Ujerumani, kwamba Arsenal wanaipambania kwa nguvu zote saini ya beki wa kati wa Bayern Munich, Kim Min-jae.

Washika Bunduki wanataka kuona usajili huo unakamilika kupitia dirisha dogo la Januari, 2027.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amepanga kuongeza nguvu kwenye eneo la beki wa kati kwa kuwa William Saliba na Piero Hincapie wako nje ya uwanja wakiuguza majeraha.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Ujerumani, Christian Falk, Arsenal wamemuweka kwenye rada zao Kim mwenye umri wa miaka 29.

Arsenal wanamini itakuwa rahisi kwao kumpata nyota huyo raia wa Korea Kusini kutokana na ukaribu wake na ofisa wao, Maurizio Micheli.

Micheli, ambaye kwa sasa ndiye anayeshughulikia usajili pale Emirates, alikuwa Napoli wakati klabu hiyo ya Italia inamsajili Kim akitokea Fenerbahce mwaka 2022.

Related articles

Recent articles