15.3 C
New York

Gilberto Mora aingia ‘18’ za Liverpool

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

KLABU ya Liverpool imeingia mazima katika mbio za kuiwania saini ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico, Gilberto Mora.

Mora ametimiza umri wa miaka 18 leo Oktoba 15, 2026, hivyo kwa sasa sheria za FIFA zinamruhusu kusajiliwa nje ya nchi.

Nyota huyo bado ana mkataba na klabu yake ya Club Tijuana ya Mexico, ambapo taarifa zinaeleza kuwa utafikia ukomo mwaka 2029.

Kwa mujibu wa mtandao wa TEAMtalk, Liverpool walianza kumfuatilia wiki mbili zilizopita, lengo likiwa ni kuinasa huduma yake wakati wa usajili wa Januari, 2027.

Aidha, klabu yake ya Tijuana imeitaka Liverpool kuandaa si chini ya Pauni milioni 30 ikiwa ni kweli ina nia ya kumsajili kinda huyo. Ada hiyo itavunja rekodi Ligi Kuu ya Mexico.

Related articles

Recent articles