23.8 C
New York

Chelsea, Arsenal zavutana kisa kiungo

Published:

LONDON, Uingereza

VIGOGO wa London, Chelsea na Arsenal, wako kwenye mchuano mkali wa kuiwania huduma ya kiungo wa Inter Milan ya Italia, Andy Diouf.

Nyota huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23, amekuwa na kiwango bora tangu Inter Milan ilipomsajili mwaka 2025 akitokea Lens ya Ufaransa.

Wakati huo huo, zipo taarifa zinazodai kuwa matajiri wa Barcelona na PSG nao wanamfuatilia kwa karibu nyota huyo.

Kwa sasa, Diouf amebakiza miaka zaidi ya mitatu katika mkataba wake na Inter, hivyo kama atauzwa, basi ni kwa euro milioni 60.

Diouf amekuwa na msaada mkubwa kwa Inter kwani mbali ya kucheza kiungo wa kati, pia amekuwa akitumika kama winga au beki wa pembeni.

Related articles

Recent articles