18.1 C
New York

Alonso akazania dili la de Jong

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Chelsea, Xabi Alonso, ameendelea kuwashinikiza mabosi wa klabu yake kumsajili kiungo wa Barcelona raia wa Uholanzi, Frenkie de Jong.

Hata hivyo, Blues watalazimika kuweka mezani kitita cha Pauni milioni 50 ili kukamilisha dili la mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa ripoti, Alonso anamtazama nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 kwenda kuziba pengo la Enzo Fernandez aliyetimkia Manchester City.

De Jong yuko nje ya dimba kwa sasa akiuguza majeraha lakini zipo taarifa zinazodai kuwa amebakiza wiki chache tu kurejea uwanjani.

Nyota huyo wa zamani wa Ajax, amekuwa Barcelona kwa miaka nane sasa, ambapo ametwaa mataji matatu ya Ligi Kuu [La Liga], likiwamo la msimu uliopita [2025-26].

Kwa sasa, bado ana mkataba na Wacatalunya hao, ikielezwa kwamba huu wa sasa utafikia ukomo mwaka 2029.

Related articles

Recent articles