LAGOS, Nigeria
SUPASTAA wa muziki wa Hip hop huko Marekani, Nicki Minaj, amelaani matukio ya kuuawa kwa waumini wa Dini ya Ukiristo nchini Nigeria.
Minaj amesema amekuwa na uhusiano wa karibu na Nigeria kwani hata mchungaji wake anatokea katika Taifa hilo la Afrika ya Magharibi.
“Kwangu binafsi, nina uhusiano na Nigeria kwa sababu mchungaji wangu anatokea Nigeria. Pia, nina mashabiki wengi kutoka huko,” amesema Minaj akiwa Texas, Marekani.
Katika hatua nyingine, Minaj aliweka wazi kuwa hatoacha kulaani kila kinachoonekana kwenda tofauti nchini humo.
Wakati huo huo, Minaj aliwataka mastaa wengine wa ndani na nje ya Nigeria kupaza sauti kulaani matukio hayo ya mauaji dhidi ya Wakiristo.


