MADRID, Hispania
KIUNGO wa kimataifa wa Croatia, Luka Modric, amekiri kuwa anatamani kurejea Real Madrid kwa gharama yoyote.
Modric aliondoka katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Hispania [LaLiga] akiwa mchezaji huru wakati wa usajili wa kiangazi mwaka 2024.
Tangu kipindi hicho, nyota huyo wa zamani wa Tottenham amekuwa akiitumikia AC Milan ya Ligi Kuu nchini Italia [Serie A].
Kwa sasa Modric ameshastaafu kuitumikia Crotia. “Nimeikumbuka Real Madrid, ni klabu ninayoipenda lakini kwa sasa najisikia vizuri nikiwa Milan. Hata hapa najisikia furaha pia,” amesema Modric.
Mkongwe huyo ameweka wazi kuwa Madrid itabaki kwenye moyo wake kwa kuwa ni klabu aliyoitumikia kwa miaka 13.


