MILAN, Italia
RIPOTI kutoka nchini Italia zinadai kuwa AC Milan inamtolea macho kiungo wa Brighton ya England, Yasin Ayari.
Usajili huo umependekezwa na kocha wa sasa wa Milan, Ruben Amorim, ambaye anataka kuimarisha safu yake ya kiungo.
Kocha huyo wa kimataifa wa Ureno anatafuta mbadala wa Luka Modric anayeweza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa 2026-27.
Amorim anahitaji sura mpya, licha ya kwamba tayari safu yake ya kiungo inao Modric, Adrien Rabiot, Yunus Musah, Ruben Loftus-Cheek, Ardon Jashari na kinda Christian Comotto.
Milan imekuwa ikimtazama kwa jicho la tatu Ayari tangu mwaka 2025, wakati huo Mkurugenzi wa ufundi akiwa ni Geoffrey Moncada.


