LONDON, Uingereza
KLABU za Manchester United, Arsenal na Chelsea ziko kwenye vita kali ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Freiburg ya Bundesliga na timu ya Taifa ya Croatia, Igor Matanovic.
Akiwa na umri wa miaka 23, nyota huyo amefunga mabao sita katika mechi saba za mashindano mbalimbali msimu huu wa 2026-27.
Msimu uliopita, pia Matanovic alikuwa moto wa kuotea mbali, ambapo alipachika jumla ya mabao 15 akiwa na kikosi hicho cha Freiburg.
Kwa upande wao, Washika Bunduki wa London wanahitaji straika mpya wa kusaidiana majukumu na Kai Havertz.
Man United wao wanatilia shaka majeraha ya mara kwa mara ya straika raia wa Slovenia, Benjamin Sesko, wakati Chelsea inataka kuwaongezea nguvu Joao Pedro na Danny Welbeck.


