CATALUNYA, Hispania
KLABU ya Barcelona inamuona staa wa Club Brugge ya Ubelgiji, Nicolo Tresoldi, kama mshambuliaji sahihi wa kusajiliwa ifikapo Januari, 2027.
Barcelona walijaribu kumsajili straika wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, wakati wa dirisha la usajili la kiangazi lililofungwa hivi karibuni lakini dili hilo liliota mbawa.
Ni baada ya dili hilo kukwama, Barcelona ilimgeukia straika kutoka Arsenal, Gabriel Jesus, ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
Vigogo hao wa Catalunya wamekuwa na uhitaji mkubwa wa mshambuliaji wa kati tangu alipoondoka nyota wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski.
Kwa siku za hivi karibuni, Raphinha raia wa Brazil amekuwa akiibeba safu ya ushambuliaji ya Barcelona, ambapo ameshafunga mabao 14 katika mechi nane.


