MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester United haijaachana na mpango wake wa kumsajili mpachikaji mabao tishio wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Man United watamgeukia kwa nguvu zote nyota huyo endapo tu watafanikiwa kumwachia Joshua Zirkzee.
‘Mashetani Wekundu’ wameuanza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu ya England [EPL] kwani wameshinda mechi moja pekee kati ya tano.
Ni kutokana na mwenendo mbaya huo, tayari kocha Michael Carrick ameingia kwenye presha kubwa ya kupoteza kibarua chake kabla ya kumalizika kwa msimu huu.
Hivi karibuni, nahodha wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand, aliishauri klabu hiyo kumsajili straika Karim Benzema, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru.


