LONDON, Uingereza
WINGA wa Chelsea, Estevao Willian, anawindwa na vigogo wa Ligi Kuu ya Hispaia [La Liga], Barcelona, licha ya kwamba huu ni msimu wake wa pili tu Stamford Bridge.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 19, amejikuta katika wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha mpya, Xabi Alonso.
Estevao mwenye umri wa miaka 19, amecheza dakika 23 pekee katika mechi nne pekee za Ligi Kuu ya England [EPL] msimu huu.
Hivyo, mchango wake kikosini umepungua kwa kiasi kikubwa, ikilinganishwa na msimu uliopita alipocheza mechi 36 na kufunga mabao nane na ‘asisti’ eight tatu.
Itakumbukwa kuwa staa huyo amerejea dimbani hivi karibuni baada ya kupona majeraha ya nyama za paja yaliyomzuia kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.


