LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ureno, Joao Felix, ameweka wazi nia yake ya kuondoka
Al-Nassr ya Saudi Arabia na kurudi katika soka la Ulaya.
Aliwahi kucheza kwa mafanikio Atletico Madrid, kabla ya kwenda kwa mkopo Barcelona, ambayo anakiri kuwa bado anatamani kuitumikia.
Joao [26], amekuwa moto wa kuotea mbali Saudia, ambapo msimu uliopita alifunga mabao 26 na kutoa ‘asisti’ 19 katika mechi 47 za mashindano mbalimbali.
Pia, nyota huyo ameendeleza moto msimu huu akiwa ameshaingia kambani mara manne na asisti tatu katika michezo yake sita aliyocheza.
“Napanga kurudi Ulaya, ingawa siyo haraka,” amesema katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha AS. “Sijui kitakachotokea mwishoni mwa msimu huu au ujao …”
Staa huyo amekuwa na mchango mkubwa pia kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa chini ya kocha Jorge Jesus kwani ndiye aliyefunga bao pekee kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wales, kisha kufunga moja walipoifunga Norway mabao 2-1.


