MILAN, Italia
LICHA ya umri wake wa miaka 46, Ronaldinho jana Novemba 15, 2026, alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Ravenna ya Italia, ambapo walishinda mabao 2-0 dhidi ya Forli.
Katika mchezo huo wa Ligi Daraja la Tatu nchini Italia [Serie C], ‘Gaucho’ alianza kikosini na ndiye aliyetoa pasi iliyokwenda kwa mchezaji aliyetoa asisti ya bao la kwanza.
Ronaldinho, ambaye alivuta hisia za mashabiki wengi uwanjani, achilia mbali kuzungukwa na waandishi wa habari kabla ya mechi, alitolewa kipindi cha pili wakati timu yake ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Staa huyo wa zamani wa PSG, Barcelona na AC Milan alionesha kiwango bora hicho, licha ya kwamba alifanya mazoezi ya siku moja tu na timu hiyo, kabla ya kupangwa jana.
Ifahamike kuwa hii ilikuwa mechi ya kwanza ya ushindani kwa kiungo mshambuliaji huyo tangu alipoachana na Fluminense ya Brazil mwaka 2015.


