LOS ANGELES, Marekani
BIBIYE Beyonce Knowles ambaye ni mke wa rapa maarufu, Jay Z, amekuwa mwanamuziki wa kwanza duniani kushiriki katika vipengele 100 tofauti kwenye historia ya Tuzo za Grammy Awards.
Hii inakuja baada ya Beyonce kuingia kwenye kipengele cha Mtumbuizaji Bora wa R&B Solo katika tuzo hizo kupitia wimbo wake wa ‘Morning Dew (Donk)’ uliotoka mwaka huu wa 2026.
Katika kipengele hicho, Beyonce mwenye tuzo 35 za Grammy, pia akiwa ni mama wa watoto watatu, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Kehlani, Victoria Monet, Jill Scott na Tems wa Nigeria.
Cha kushangaza, anayefuata katika nafasi ya pili kwa kuwahi kuwania vipengele vingi kwenye historia ya Grammy ni mumewe, Jay-Z, ambaye ana ameshiriki mara 90.
Tuzo za Grammy, ambazo ni za 69 tangu kuanzishwa kwake, zinatarajiwa kutolewa Februari 7, 2027, nchini Marekani.


