13.1 C
New York

Kocha Ureno ‘ampotezea’ mama yake Ronaldo

Published:

LISBON, Ureno

LICHA ya mama yake Cristiano Ronaldo kumkosoa, kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Ureno ameonesha kutokwazika na maneno ya ‘bi mkubwa huyo’.

Kwa wiki za hivi karibuni, Jesus na Ronaldo wamekuwa wakiripotiwa kutokuwa na uhusiano mzuri, kiasi cha supastaa huyo wa soka kuamua kustaafu kuitumikia timu ya taifa.

Juzikati, mama yake Ronaldo, Dolores Aveiro, alisema wazi kwamba amefurahi kuona Ureno ikitandikwa mabao 4-1 na Denmark.

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mechi yao dhidi ya Wales itakayochezwa kesho Novemba 17, 2026, Jesus amesema anaelewa hisia kali alizonazo mama huyo juu ya mwanaye.

“Naelewa kile alichokisema mama yake Cristiano Ronaldo. Mwisho wa siku, mama ni mama tu,” amesema Jesus mwenye umri wa miaka 72.

“Kwa namna nilivyosoma, alimkuza mtoto wake kwenye mazingira magumu. Ni mama ambaye ni mfano wa kuigwa. Kwa hiyo, kwa upande wangu, naelewa.”

Related articles

Recent articles