Na Editha William, Gazetini- KAGERA
TIMU ya soka ya Fenicha FC imevuna sare nyingine katika mchezo wake wa pili wa michuano ya Muhaj Cup 2026 inayoendelea Kata ya Hamgembe iliyoko Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.
Katika mchezo huo, Kashabo FC ilivaana na Furniture FC, ambapo timu hizo zilitoa sare ya kutokufungana [0-0], hivyo kila moja kuondoka na pointi moja.
Dakika 90 za mechi hiyo ziliishuhudia Kashabo FC ikimaliza pungufu baada ya mmoja wa wachezaji wake kulimwa kadi nyekundu.
Kwa matokeo hayo, sasa Fenicha inafikisha pointi mbili, wakati Kashabo FC wao wakiwa wameshakusanya pointi nne baada ya mechi mbili.
Wakati huo huo, mchezo mwingine ni ule uliozikutanisha Mchikichini FC na Omukishenye FC, ambao pia ulimalizika kwa timu hizo kugawa pointi baada ya sare ya mabao 2-2.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Injinia Johnston Johansen Mutasingwa, ameendelea kuonesha sapoti yake katika michezo baada ya kutoa katoni za maji kwa kila timu.


