7.3 C
New York

Salah aandika historia mpya Misri

Published:

CAIRO, Misri

MKONGWE wa Liverpool, Mohamed Salah, ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya soka ya Taifa ya Misri baada ya kufunga mabao mawili jana Novemba 13, 2026.

Salah aliingia kambani mara mbili wakati Misri ilipoibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kufuzu fainali zijazo za AFCON 2027.

Nyota huyo wa Trabzonspor ya Uturuki alifunga bao la kwanza na kufikia rekodi ya Hossam Hassan, kabla ya kuivunja kwa bao la pili kwa penalti ya kiufundi aliyoipiga kwa staili ya ‘Panenka’.

Hivyo, ameshafikisha mabao 70, akifuatiwa na Hossam Hassan [69], Hassan El-Shazly [49], El-Sayed El-Dhizui [41], na Mohamed Aboutrika [38].

Ikumbukwe, Salah alianza kuitumikia Misri mwaka 2011 na tayari staa huyo mwenye umri wa miaka 34 ameshacheza mechi 123 akiwa na kikosi hicho.

Related articles

Recent articles