8.3 C
New York

Gamondi afunguka Stars kutandikwa ugenini

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR

KOCHA wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Miguel Gamondi, amekiri kuwa tofauti kubwa ya ubora kati yao na Nigeria ndiyo iliyosababisha watandikwe mabao 3-1 jana Novemba 13, 2026.

Gamondi ameibuka na kauli hiyo baada ya Stars kupoteza mchezo huo wa ugenini wa kufuzu fainali za AFCON 2027.

Akihojiwa na televisheni ya mtandao ya Shirikisho la Soka nchini [TFF], kocha huyo wa kimataifa wa Argentina amesema: “Napenda kuwapongeza wachezaji wangu kwa namna walivyopambana, kujitoa kwao, walivyokimbia, walijitoa kweli kweli.

“Tulijua wazi kuwa tunacheza dhidi ya timu kubwa, tulifanya kosa kubwa ndani ya dakika mbili tu za mchezo lakini tuliweza kusawazisha na kwenda mapumziko tukiwa sare [1-1].”

Katika hatua nyingine, Gamondi amesema kilichotokea katika mechi hiyo ni somo kwa wachezaji wake kuelekea mechi zinazofuata.

“Tunapaswa kuwapongeza Nigeria, kwangu hii ni moja ya timu bora Afrika na Tanzania inapaswa kuendelea kujifunza kwa sababu mechi ya aina hii inatupa somo na kuona tulipofika,” amesema.

Related articles

Recent articles