LOS ANGELES, Marekani
MWIGIZAJI wa Marekani aliyepata jina kubwa kupitia filamu ya ‘Prison Break’, Stacy Keach, amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
Aliyetangaza kifo chake ni mkewe, Małgosia Tomassi Keach, akimtaja mwigizaji huyo kuwa ni mwigizaji aliyevutiwa mamilioni ya watu duniani kote.
Keach alifanya vizuri akitumia jina Henry Pope katika tamthilia hiyo iliyovuta watazamaji wengi wa ndani na nje ya soko la filamu la Marekani [Hollywood].
Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo wa filamu alifariki jana Novemba 11, 2026, akiwa nyumbani kwake mjini Magdalenka, Poland.
Ripoti zinaeleza kuwa Keach amepoteza maisha baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani na moyo.
Alianza uigizaji katika miaka ya 1960 lakini aliingia rasmi kwenye soko la filamu katika miaka 1970.


