18.3 C
New York

Mwimbaji wa ‘gospo’ aweka rekodi YouTube

Published:

LAGOS, Nigeria

NATHANIEL Bassey amekuwa mwimbaji wa kwanza wa muziki wa Injili barani Afrika kufikisha zaidi ya watazamaji bilioni moja katika mtandao wa kijamii wa YouTube.

Mbali ya kufikisha watazamaji 1,014,544,577, Bassey ambaye pia ni mchungaji, ameweza kuwa na wafuatiliaji [subscribers] milioni 5.24 kwenye chaneli yake ya YouTube tangu ilipoanzishwa mwaka 2011.

Chaneli yake ya YouTube imepewa nguvu zaidi kutokana na uwepo wa nyimbo zinazofanya vizuri, zikiwamo ‘Imela’, ‘You Are God’ na ‘Onise lyanu’.

Mafanikio yake hayo yamepokewa kwa shangwe na mashabiki wake, ambao wamefurika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kumpongeza.

Related articles

Recent articles