LAGOS, Nigeria
BIBIYE mwenye jina kubwa katika soko la filamu za Nigeria [Nollywood], Rachael Okonkwo, amevishwa pete na mchumba wake ambaye ni bilionea, Chukwudi Onuorah.
Kwa mujibu wa ripoti, Okonkwo alivishwa pete katika hafla fupi na ya kihafari iliyofanyika wikiendi iliyopita.
Okonkwo ni mmoja ya waigizaji wa kike wenye ushawishi mkubwa katika soko la filamu la Nigeria, akifahamika kwa kazi zake zinazofanya vizuri sokoni.
Alianza kujizolea umaarufu kwenye tasnia ya uigizaji mwaka 2014 baada ya kazi nzuri aliyoifanya katika muvi iitwayo ‘Nkoli Nwa Nsukka’.


