MILAN, Italia
MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Alphadjo Cisse, alitupia ‘hat trick’ katika ushindi wao wa mabao 4-0 dhidi ya RB Salzburg, mchezo wa Ligi ya Europa uliochezwa jana Oktoba 15, 2026.
Akiwa na umri wa miaka 19 na siku 358, Cisse amekuwa mchezaji mdogo zaidi raia wa Italia kufunga mabao matatu ya mchezo mmoja wa michuano ya Ulaya [Europa na Ligi ya Mabingwa].
Kabla ya kuvunja rekodi hiyo, Giancarlo Danova ndiye aliyekuwa akiishikilia baada ya kufunga ‘hat trick’ akiwa na umri wa miaka 20 na siku 309.
Wakati huo huo, Cisse amekuwa mchezaji wa kwanza wa Milan kufunga hat trick katika mechi ya michuano ya Ulaya tangu Filippo Inzaghi alipofanya hivyo dhidi ya Deportivo La Coruña nmwaka 2002.
“Nimefurahishwa sana na ‘hat trick’ hii, pamoja na ushindi pia,” amesema Cisse na kuongeza: “Nimefurahi na nitaendeleza kiwango bora hiki katika mechi zijazo.”


