18.3 C
New York

Chelsea yamkodolea macho Vuskovic

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Chelsea imeanza harakati za kuinasa saini ya beki wa kati wa zamani wa Tottenham, Luka Vuskovic.

Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia amekuwa kwenye kiwango bora tangu aliposajiliwa na Brighton wakati wa usajili uliopita wa majira ya kiangazi, 2026.

Lakini, inafahamika kuwa Blues watalazimika kuweka mezani kitita cha zaidi ya Pauni milioni 50 ili kuinasa huduma ya nyota huyo.

Mwandishi wa habari za michezo wa Uingereza, Ekrem Konur, Chelsea imemuongeza Vuskovic katika orodha ya mabeki inaowataka ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, huenda isiwe rahisi kihivyo kwani saini ya mlinzi huyo pia imekuwa ikitolewa macho na klabu zingine kubwa, zikiwamo Barcelona, Bayern Munich na Real Madrid.

Related articles

Recent articles