18.1 C
New York

Baba: Merino yupo sana Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

BABA mzazi wa kiungo wa Arsenal, Mikel Merino, amezipuuzia tetesi zinazomuhusisha mtoto wake na Real Madrid, akisisitiza kuwa ataendelea kukipiga Emirates.

Merino mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na Washika Bunduki hao wa London mwaka 2024 akitokea Real Sociedad, usajili huo ukigharimu kitita cha Pauni milioni 31.6.

Wakati huo, Madrid walijaribu kuinasa saini yake lakini dili liliota mbawa baada ya mchezaji huyo kuchagua kuondoka La Liga na kuchagua kuvaa jezi ya Arsenal.

Tangu alipojiunga na Arsenal ya kocha Mikel Arteta, Merino amecheza mechi 86 za mashindano mbalimbali, akifunga mabao 16 na kutoa asisti nane.

Hata hivyo, msimu huu wa 2026-27 haujawa mzuri kwa nyota huyo kwani hajaingia kikosi cha kwanza katika mechi yoyote ya Ligi Kuu ya England [EPL].

Akizungumzia juu ya tetesi za kuhusishwa na Madrid, baba yake amesema: “Kwa sasa ni mchezaji wa Arsenal na ametwaa taji la Ligi Kuu ya England, amefika nusu fainali na fainali ya Ligi ya Mabingwa.”

Related articles

Recent articles