18.3 C
New York

Arsenal macho kwa kinda Hispania

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Arsenal iko kwenye mawindo ya kiungo wa pembeni wa Granada ya Hispania, Owen Emeka.

Wakati huo huo, Newcastle United na Everton ni klabu zingine za England zilizoonesha nia ya kumsajili kinda huyo mwenye umri wa miaka 17.

Emeka anayetokea pembeni [winga ya kulia], ameshacheza mechi sita akiwa na kikosi cha timu ya wakubwa ya Granada inayoshiriki Ligi Daraja la Pili [Segunda].

Septemba 12, 2026, mchezaji huyo alifunga bao lake la kwanza akiwa na timu ya wakubwa ya Granada katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Albacete.

Kwa upande mwingine, ameshacheza mechi mbili akiwa na kikosi cha U-18 ya Hispania, ikiwamo ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brazil.

Kwa sasa, kinda huyo ana mkataba na Granada utakaofikia ukomo mwishoni mwa msimu wa 2030-31. Timu hiyo inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Segunda ikiwa na pointi nane tu katika mechi saba.

Related articles

Recent articles