12.8 C
New York

Arsenal wamtolea macho Haaland

Published:

LONDON, Uingereza

ARSENAL na Real Madrid zimeingia kwenye mbio za kuiwania saini ya mpachikaji mabao hatari wa klabu ya Manchester City, Erling Haaland.

Taarifa zinaeleza kuwa kila upande umepiga hatua kwa kuwasiliana na wawakilishi wa straika huyo wa kimataifa wa Norway.

Hayo yanakuja wakati huu klabu ya Man City ikikabiliwa na mashitaka zaidi ya 100, ikiwamo kukiuka nidhamu ya matumizi ya fedha.

Hata hivyo, klabu hizo zitalazimika ‘kuvunja kibubu’ kwani mkataba wake na mabosi wa Etihad utafikia ukomo mwaka 2034. Mkataba huo hauna kipengele kinachoiruhusu Man City kumuuza.

Haaland ameendeleza moto wake msimu huu wa 2026-27 kwani ameshaifungia Man City jumla ya mabao saba. Pia, amepachika mawili akiwa na Norway katika michuano ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya [UEFA Nations League].

Related articles

Recent articles