2 C
New York

Kamati ya Bunge yaridhishwa na kiwanda cha nguzo za zege Tabora

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi na kuanza kwa uzalishaji katika Kiwanda cha Zege kinachomilikiwa na kampuni tanzu ya Tanesco, kinachozalisha nguzo za zege mkoani Tabora.

Akizungumza baada ya ziara ya kikazi ya kamati hiyo Machi 12, 2026, Mwenyekiti wa Kamati, Subira Mgalu, amesema wamefurahishwa na hatua ya kukamilika kwa kiwanda hicho na kuanza kwa uzalishaji.

“Kwa niaba ya Kamati tumeridhika na kazi kubwa iliyofanyika katika kiwanda hiki. Tunatoa rai kwa Wizara ya Nishati na Tanesco kuhakikisha wanakisima mia kiwanda hiki ili kiendelee kufanya kazi kwa ufanisi na kuzalisha faida,” amesema Mgalu.

Ameongeza kuwa serikali inaelekea kuhamia zaidi katika matumizi ya nguzo za zege badala ya nguzo za miti, hasa katika maeneo yenye unyevunyevu, karibu na mito au misitu ambako nguzo za miti huathiriwa kwa urahisi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kiwanda hicho kilianza uzalishaji rasmi Februari 2026 na kwa sasa kina uwezo wa kuzalisha nguzo kati ya 80 hadi 120 kwa siku.

Ameeleza kuwa hadi kufikia hatua ya kuanza uzalishaji, jumla ya Sh bilioni 6.4 zimetumika katika ujenzi wa kiwanda hicho, huku zaidi ya Sh bilioni 1.6 zikiwa bado hazijalipwa kwa mkandarasi ambaye bado yupo katika kipindi cha uangalizi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Lazaro Twange, amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kuongeza upatikanaji wa nguzo za zege na kuboresha huduma ya umeme nchini.

Amesema matumizi ya nguzo za zege ni teknolojia inayokua kwa kasi na shirika hilo linaendelea kuwekeza ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa nguzo za kutosha kwa ajili ya miradi ya kusambaza umeme kwa wananchi.

Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imelenga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati inayotekelezwa na Tanesco katika maeneo tofauti nchini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img