LONDON, Uingereza
KLABU za Arsenal na Chelsea zimepata pigo kubwa baada ya watu wa karibu wa Julian Alvarez kusema nyota huyo anaitaka Barcelona.
Ripoti zilizopo zinaeleza kuwa Alvarez anahusishwa na mpango wa kuondoka Atletico Madrid mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester City amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipotua Atletico mwaka 2024 kwa ada ya Pauni milioni 81.8.
Akiwa na umri wa miaka 26 kwa sasa, Alvarez aliondoka Etihad kwa kushindwa kupambania namba mbele ya Erling Haaland.
Chini ya kocha Diego Simeone, Alvarez alifunga mabao 29 katika msimu wake wa kwanza (2024-25) klabuni hapo.
Msimu huu wa 2015-26, Alvarez ameshaingia kambani mara 12 na kutoa ‘asisti’ saba katika mechi 37 alizocheza.


