MANCHESTER, Uingereza
UNAMKUMBUKA beki wa zamani wa Manchester United, West Brown? Alisifika kwa ‘ukatili’ wake ndani ya uwanja, hasa kwa washambuliaji tishio aliokabidhiwa kuwadhibiti.
Brown aliyezaliwa mjini Manchester, alikuwa sehemu ya ‘kizazi cha dhahabu’ cha Man United, ambapo alitwaa mataji matano ya Ligi Kuu (EPL) akiwa na Man United.
Sasa, mlinzi huyo wa zamani wa timu ya taifa England amesema kwa sasa haoni mshambuliaji wa kufikia kiwango alichokuwa nacho Wayne Rooney.
“Sijawahi kuona mchezaji wa kumfikia Rooney tangu alipostaafu. Na sioni kama atatokea kwa sababu alikuwa wa pekee sana,” amesema Brown.
Kwa upande mwingine, Brown anajaribu kumfananisha Rooney na mshambuliaji tishio wa sasa wa England, Harry Kane.
“Si mchezaji aina ya Harry Kane kwa sababu Rooney si mshambuliaji anayekaa kwenye boksi,” amesema.


