3.2 C
New York

Nigeria yaipiga Misri mshindi wa tatu AFCON 2025

Published:

CASABLANCA, Morocco

TIMU ya taifa ya Nigeria ‘Super ‘Eagles’ imeshika nafasi ya tatu msimu huu wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) baada ya kuifunga Misri kwa penalti 4-2, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Mohammed V.

Mechi hiyo imechezwa Januari 17, 2026, ambapo dakika za uwanjani zilimalizika kwa matokeo ya timu hiyo kutokufungana.

Nigeria walipata bao la kuongoza dakika ya 39 kupitia kwa Akor Adams lakini lillikataliwa baada ya VAR kuonesha kuwa staa mwenzake, Paul Onuachu, kumpiga kiwiko Hamdy Fathy wakati wa shambulizi hilo.

Katika hatua ya penalti, kipa wa Nigeria, Stanley Nwabali, aliokoa mbili za mwanzo za Mohammed Salah na Omar Marmoush.

Misri, mabingwa mara saba wa michuano ya AFCON, waliangukia katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu baada ya kufungwa bao 1-0 na Senegal katika hatua ya nusu fainali.

Kwa upande wao, Super Eagles nao waliishia nusu fainali baada ya kufungwa mabao 2-0 na wenyeji wa mashindano ya msimu huu, Morocco.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img