2.9 C
New York

Azam hoi, yapigwa tena Shirikisho

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
BAO pekee la dakika ya 57 la Nordin Amrabat liliipa Wydad Casablanca uhakika wa pointi tatu za mchezo wao wa ugenini dhidi ya Azam FC.
Mechi hiyo ya Kundi B msimu huu wa Kombe la Shirikisho Afrika ilichezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Kwa matokeo hayo, Wydad iko kileleni ikiwa na pointi sita baada ya ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Nairobi United.
Azam ya kocha Florent Ibenge haijakusanya pointi yoyote hadi sasa kwani mechi yao ya kwanza waliyokuwa ugenini walifungwa mabao 2-0 na Maniema Union ya DRC.
Hivyo basi, katika msimamo wa Kundi hilo, Wydad iko kileleni ikiwa na pointi sita, ikifuatiwa na Maniema yenye pointi tatu.
Aidha, Nairobi United na Azam ziko katika nafasi ya tatu na ya nne, kila moja ikiwa haijaonja ushindi wala sare katika mechi mbili zilizopita.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img