2.9 C
New York

Yanga kutamba ugenini leo?

Published:

KABYLIA, Algeria
YANGA watakuwa ugenini leo kumenyana na JS Kabylie, mchezo wa pili kwa kila timu msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ni mechi ya Kundi B, ambalo kinara ni Al Ahly yenye pointi tatu, sawa na Yanga inayoshika nafasi ya pili.
‘Timu ya Wananchi’ ilipata pointi tatu hizo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Kwa upande wao, JS Kabylie walipoteza mechi yao ya kwanza walipofungwa mabao 4-1 na Al Ahly, mchezo uliochezwa mjini Cairo, Misri.
JS Kabylie inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Algeria ikiwa na pointi 15, sawa na CS Constantine iliyoko kileleni.
Hata hivyo, imecheza mechi tisa, tofauti na Constantine ambayo imeshashuka dimbani mara 11.
Katika michezo tisa hiyo, JS Kabylie imshina minne, imefungwa miwili na kupata sare tatu.
Wakati Yanga wakimenyana na JS Kabylie, leo pia Al Ahly watakuwa ugenini nchini Morocco kumenyana na AS FAR.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img