2.9 C
New York

Viwango vipya CAF, Simba nafasi ya tano

Published:

CAIRO, Misri
RIPOTI mpya ya viwango vya ubora wa klabu vya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) imetoka na Simba ya Tanzania iko nafasi ya tano.
‘Wekundu wa Msimbazi’ ameshika nafasi hiyo baada ya kukusanya pointi 48, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Wakati Simba ikiwa hapo, Al Ahly FC ya Misri iko kileleni (pointi 78), ikifuatiwa Mamelodi Sundowns (62), Esperance (57), na RS Berkane (52).
Nafasi ya sita imeangukia kwa Pyramids FC (47), ikifuatiwa na Zamalek SC (42), Wydad AC (39), USM Alger (37), na CR Belouizdad (36).
Viwango hivyo vinatokana na mafanikio ya klabu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kwa misimu mitano iliyopita, kabla ya huu wa 2025-26.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img