MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Trabzonspor ya Uturuki imewasiliana na wakala wa Andre Onana na kumwambia inataka kumsajili moja kwa moja kipa huyo wa Manchester United.
Onana alijiunga na Trabzonspor kwa mkopo akitokea Old Trafford na sasa klabu hiyo imenogewa na uwezo aliouonesha kwa wiki chache za hivi karibuni.
Katika mechi nne alizosimama langoni, mbili zilimalizika bila kipa huyo raia wa Cameroon kuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Kwa mujibu wa taarifa, kocha wa Fatih Tekke amewasilisha ombi kwa mabosi wa Trabzonspor akiwataka kumbakiza Onana.
Hata hivyo, katika makubaliano ya awali kati ya Man United na Trabzonspor hakuna kipengele kinachowaruhusu Waturuki hao kumsajili moja kwa moja.
Onana harudi Man United
Published:


