4.1 C
New York

Maandamano ya kumng’oa Rais yashika kasi Serbia

Published:

MAELFU ya wanafunzi na wanaharakati nchini Serbia wameandama wakishinikiza uchaguzi mkuu wa haraka ili kumng’oa madarakani Rais Aleksandar Vucic.

Huu ni mwendelezo wa miezi mingi ya hivi karibuni iliyoshuhudia maandamano ya wengi wanaoupinga utawala wa Rais Vucic wakiutaja kuminya uhuru wa kujieleza, ikiwamo kuwapa wakati mgumu wanasiasa wa upinzani.

Maandamano ya leo (Jumamosi) mjini Belgrade hayatofautiani na yaliyopita kwani yanashinikiza uchaguzi wa haraka, licha ya kwamba Rais huyo aliyeiongoza Serbia kwa miaka 12 kuachia ngazi atamaliza muda wake mwaka 2027.
Kutokana na ukubwa wa maandamano hayo, polisi walilazimika kuzingira na kudumisha ulinzi katika maeneo muhimu, yakiwamo majengo ya Serikali na Bunge.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img