1.4 C
New York

Chart| Mwenendo wa Utekelezaji wa Mradi wa JNHPP

Published:

Na Jackline Jerome, Gazetini

Tanzania inatekeleza ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa
MW 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Bwawa la Julius Nyerere(JNHPP).

Gharama ya mradi huu
ni Sh trilioni 6.55 ambazo zinagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.

Hadi kufikia Aprili, 2023 utekelezaji wa mradi huu katika maeneo yote kwa ujumla ulifikia asilimia 86.89 kutoka asilimia 60.22 zilizokuwa zimefikiwa Aprili, 2022 na mradi unatarajiwa kukamilika Juni, 2024.

Kulingana na Hotuba ya Waziri wa Nishati, January Makamba akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi yawizara hiyo kwa mwaka 2023/2024, hadi kufikia Mei 23, 2023 kiwango cha maji kimefikia mita za ujazo bilioni 11.8 sawa na asilimia 39.3 ya kiwango cha juu ambacho ni mita za ujazo bilioni 30.

Zaidi angalia mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa JNHPP kuanzia Aprili, 2022 hadi Aprili, 2023 kupitia usanifu wetu hapo juu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img