Kwa mujibu wa Matokeo Muhimu ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2015-16, yanaonyesha kuwa asilimia 9 ya wanaume wa Tanzania wana mke zaidi ya mmoja.
Utafiti huo unabainisha kuwa ndoa za mitala pia ni nyingi zaidi kwa wanaume katika kaya maskini sana kwa asilimia 13.
Aidha, umebainisha kuwa asilimia 18 ya wanawake wa Tanzania wapo katika ndoa za mitala, ikiwa na maana kwamba wana mke mwenza angalau mmoja.
Pia ndoa za mitala zipo nyingi zaidi kwa wanawake wasio na elimu elimu kwa asilimia 31, katika kaya maskini sana ni asilimia 29 na maeneo ya vijijini ni asilimia 21.