2 C
New York

Trinity Rodman; Mchezaji ghali zaidi soka la wanawake duniani

Published:

LONDON, Uingereza

MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya taifa ya Marekani, Trinity Rodman, amekuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani kwa upande wa soka la wanawake.

Rodman, ambaye ni binti wa staa wa zamani wa Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), Dennis Rodman, ameweka rekodi hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Washington Spirit.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, amekuwa mchezaji huru tangu alipomaliza mkataba wake na Spirit mwishoni mwa mwaka 2024.

Kwa mujibu wa wakala wake, Rodman amesaini mkataba mpya wenye thamani ya Dola za Marekani Dola za Marekani milioni 2, zikiwamo posho. Ataitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2028.

Kabla ya Rodman, mchezaji aliyekuwa akiongoza kwa kulipwa vizuri zaidi duniani kwa upande wa soka la wanawake alikuwa Aitana Bonmati wa Barcelona.

Bonmati, anafahamika kwa rekodi yake ya kuibeba mara tatu mfululizo tuzo ya Ballon d’Or, akifanya hivyo nwaka 2023, 2024 na 2025.

Safari ya maisha ya soka ya Rodman ilianza tangu akiwa na umri wa miaka minne. Mama na dada yake ndiyo waliokuwa wakimuunga mkono katika kupambania ndoto zake za kuwa staa wa kandanda.

Hata hivyo, jina lake lilianza kupata umaaarufu mkubwa mwaka 2021, baada ya kuiongoza Spirit kutwaa taji la Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake ya Marekani (NWSL).

Ni mwaka ambao alitwaa pia tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu hiyo. Alianza kuitumikia timu ya taifa mwaka 2022, kipindi ambacho alifunga mabao 11.

Wakati wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 2024 jijini Paris, Ufaransa, Rodman alifunga mabao matatu na Marekani ilitwaa ubingwa.

Kwa upande wa baba yake, aliwahi kuwika NBA, ikiwa ni pamoja na kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu hiyo akiwa na Pistons na Chicago Bulls.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img