7.9 C
New York

Ronaldo nje Kombe la Dunia?

Published:

RIYADH, Saudi Arabia

MSHAMBULIAJI wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, atakuwa nje ya dimba kwa muda na hiyo imezua hofu kuwa huenda akazikosa fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazoanza Juni, 2026.

‘CR7’ alishindwa kumaliza dakika 90 za mchezo wao wa Februari 28, 2026 dhidi ya Al-Fayha, ambapo Al Nassr walishinda mabao 3-1.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia, staa huyo wa timu ya taifa ya Ureno alitolewa dakika ya 81 baada ya kupata maumivu ya misuli.

Kocha wa Al Nassr, Jorge Jesus, amesema Ronaldo mwenye umri wa miaka 41 amepata majeraha ya misuli katika paja la mguu wake  wa kulia.

Awali, ilionekana angerejea mapema uwanjani lakini sasa kuna hofu kuwa nyota huyo atakuwa nje kwa muda mrefu zaidi.

“Baada ya vipimo, tumeona majeraha ya Cristiano Ronaldo ni makubwa zaidi kuliko tulivyotarajia,” amesema Jesus.

“Cristiano atasafiri kwenda Hispania, kama wachezaji wengine wanavyokwenda kwa matibabu baada ya majeraha.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img