7.9 C
New York

Evra awavaa Scholes, Neville kisa Carrick

Published:

MANCHESTER, Uingereza

BEKI wa zamani wa Manchester, Patrice Evra, amewatolea uvivu wakongwe wenzake wa timu hiyo, Paul Scholes, Gary Neville na Roy Keane, akiwaambia waache ‘kumzingua’ Michael Carrick.

Baada ya Man United kutandikwa mabao 2-1 na Newcastle United hivi karibuni, Scholes alikuwa wa kwanza kukosoa kiwango cha timu hiyo katika mchezo huo wa Ligi Kuu.

Kwa upande wa Evra, amedai kuwa ukosoaji wa mara kwa mara unaofanywa na wakongwe wa Man United unaweza kumuharibia Carrick.

“Nadhani alichoandika Scholes ni feki, labda akaunti yake ya Instagram ilidukuliwa,” amesema Evra akihojiwa na Gazeti la Daily Mail.

Aidha, Mfaransa huyo amedai kushangazwa na tabia ya Scholes tangu alipostaafu kucheza na kugeukia uchambuzi wa kandanda.

“(Scholes) alikuwa mchezaji asiye na maneno mengi enzi zake uwanjani lakini siku hizi amekuwa akibwatuka kwenye vyombo vya habari.

“Sijui kwanini hawamuungi mkono Michael Carrick, ni mwenzetu na anafanya vizuri,” amesema Evra.

Katika hatua nyingine, Evra aliyekuwa akicheza beki wa pembeni amekumbusha Neville alivyofeli katika kazi ya ukocha akiwa Valencia, pia Scholes alipojaribu kuinoa Oldham.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img