2.9 C
New York

Biteko akabidhi ofisi, aahidi kuendeleza ushirikiano

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

ALIYEKUWA Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko leo 20 Novemba, 2025 amemkabidhi  rasmi ofisi Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi.

Ndejembi amekabidhiwa ofisi hizo zilizoko Mtumba mkoani Dodoma ambapo amemshukuru Dk.Biteko kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote cha uongozi wake.

Amesema katika kipindi cha uongozi wake, utendaji kwenye sekta ya nishati umekuwa kwa kiasi kikubwa na huduma za utendaji zimeboreshwa na tija kuonekana katika harakati za kukuza sekta ya nishati.

Waziri Ndejembi ameahidi atayaendeleza yote pale alipoishia  Dk. Biteko, ili kuhakikisha azma ya serikali na maono iliyonayo kufanikisha miradi ifikapo 2030.

Kwa upande wake, Dk. Biteko amempongeza Ndejembi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na kumhakikishia kumpa ushirikiano wakati wowote katika kufanikisha maono makubwa ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Nishati.

“Mengi niliyojifunza kipindi nikiwa Wizara ya Nishati lakini jambo kubwa zaidi ni sala zangu kwenu katika utekelezaji wa kazi zenu za kila siku,” amesema Biteko. 

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img