18.7 C
New York

Tanzania, Zambia zakutana kujalidili  uimarishaji mpaka

Published:

Na Mwandishi Wetu

Kikao cha Kamati ya pamoja cha wataalamu wa Tanzania na Zambia kimeanza mkoani Songwe , kujadili mpango kazi wa uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo.


Kikao hicho kimeanza  Mei 5, 2025 na kutaratarajiwa kumalizika Mei 9, 2025 katika mji wa Tunduma mkoani Songwe na kuhusisha wataalamu kutoka nchi  hizo mbili.

Akifungua kikao hicho cha siku tano, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amesema, Tanzania imejipanga kikamilifu kutekeleza zoezi la uimarishaji mpaka wa kimataifa kwa ajili ya ustawi wa nchi hizo.

“Uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Zambia una lengo la kuweka usimamizi mzuri wa mpaka baina ya nchi hizo pamoja na kukuza amani, upendo, usalama na maisha ya watu wake,” amesema Chongolo.

“Ni imani yangu kila mshiriki katika kikao hiki atatumia muda kuhakikisha uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi zetu unakuwa na matokeo mazuri kwa ustawi wa nchi na wananchi wetu,” amesema.

Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni kiongozi wa timu ya Tanzania kwenye kikao hicho, Hamdouny Mansoor amesema, mkutano huo ni utekelezaji wa mpango wa Umoja wa Afrika kuhusu uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa nchi za Afrika kufikia mwaka 2027.

 ” Ni nia ya Umoja wa Afrika kuzifanya nchi za Afrika kuwa na amani pasipo migongano wakati wa zoezi zima za uimarishaji mipaka ya kimataifa,” amesema Mansoor .

Mpaka wa Tanzania na Zambia una urefu wa takriban km 345 ambapo km 100 ni nchi kavu, km 189 ni mto Kalambo na km 56 ziwa Tanganyika

Tanzania imepakana na nchi 10 ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, DRC, Zambia, Malawi, Msumbiji, Comoro na Shelisheli huku mipaka baina ya nchi hizo ikiwa imegawanyika katika sehemu mbili za nchi kavu na majini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img