19.1 C
New York

Rais atangaza kifo cha Cleopa Msuya

Published:

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan  ametangaza kifo cha aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa  Rais na Waziri Mkuu,   Cleopa Msuya  kilichotokea leo Mei 7, 2025 katika

hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.

Akitangaza msiba huo, Rais Samia amesema  Mzee Msuya alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo kwa kipindi kirefu na alipata matibabu ya nchini katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Mzena na nje ya nchi London, Uingereza.

“Natoa pole kwa familia, ndugu na jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa, natangaza siku saba za maombolezo kuanzia tarehe 7-13 ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti,” amesema Rais Samia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img