19 C
New York

Nzali Next Level kuendelea kupambania Injili ya Kiswahili Marekani, Flora Mayala kutikisa Dallas

Published:

Na Mwandishi Wetu,Gazetini

Mdau maarufu wa burudani nchini mwenye makazi yake nchini Marekani, Lonely Nzali, ameendelea kusapoti muziki wa Injili Afrika Mashariki kupitia majukwaa yake ya Swahili Gospel Promotion, Nzali Next Level na Diaspora Magazine.

Nzali ambaye ni mtangazaji wa mkongwe ,amewekeza nguvu kubwa katika kuwasapoti waimbaji wa injili na wahubiri mbalimbali wa kutoka Tanzania nchini Marekani.

Akizungumza na Gazetini.co.tz, Nzali ambaye kwa sasa yupo na mwimbaji nyota wa Injili nchini, Flora Mayala (Madame Flora) huko Marekani, amesema kiu yake ni kuona waimbaji wa Kitanzania wanajihisi wapo nyumbani wanapokuwa kwenye huduma ughaibuni.

“Nimekuwa nikiwapokea waimbaji wengi wa Tanzania wanapokuja hapa Marekani, sasa hivi nipo na Flora Mayala na ana ziara ndefu kwenye miji mbalimbali akiendelea na huduma, mfano kesho Jumapili atakuwa hapa Umoja Internatinal Outreach Church kwa Pastor Dr Absalom Nasuwa na mhubiri mkuu Dr Zakayo Nzogele,” amesema Nzali.

Flora ameingia kwenye orodha ndefu ya waimbaji wa Injili wa Tanzania ambao Nzali Next Level imewapa sapoti wanapokuwa kwenye huduma zao ughaibuni, wengine ni Dr Ipyana, Boaz Danken, Paul Clement, Joel Lwaga na wengine kibao.

Nzali ameongeza kuwa kupitia tovuti yake ya https://nzalinextlevel.wixsite.com/the-diaspora-magaz-1 ataendelea kusapoti Injili ya Kiswahili nchini Marekani kadiri Mungu alivyomjalia kuunganisha watu wengi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img